Monday, December 23, 2024
Home > Counties > Nakuru > Wanawake 5 mahakamani kwa kushiriki ukeketaji

Wanawake 5 mahakamani kwa kushiriki ukeketaji

Mahakama ya Molo imewaachilia wanawake 5 kwa dhamana ya Sh.200, 000 kila mmoja kwa kushiriki katika tohara za wanawake kinyume na sheria.

Sharon Mutai, Martha Cheruiyot, Mercy Cheruiyot, Lorna Cheruiyot na Viola Rono walishtakiwa kwa kutenda kitendo hiki mnamo Novemba 23 mwaka huu, katika lokesheni ya Kamara iliyoko katika kaunti ndogo ya Molo,  na pia kukosa kutoa habari hizi kwa maafisa wa polisi.

Martha Cheruiyot alikabiliwa na shtaka lingine la kuitumia nyumba yake kama mahala kwa kufanyia ukeketaji.

Wakiwa mbele ya hakimu mkazi, Alice Mukenga, walikana madai haya.

Inasemekana kuwa wakazi walishirikiana kutoa habari kwa maafisa wa serikali pale walipojua kuwa mila hii potovu na ambayo haikubaliki kisheria ilikuwa ikiendelezwa.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 30, 2020 itakaposikilizwa.

Na  Emily  Kadzo

Leave a Reply