Thursday, December 26, 2024
Home > Counties > wakaazi wa Tana River wahimizwa kuhifadhi wanyama pori

wakaazi wa Tana River wahimizwa kuhifadhi wanyama pori

Waziri wa Utalii, Kaunti (CEC) ya Tana River, Yahya Burrow, alalamikia uwindaji haramu haswa wa wanyama wadogo wadogo wa pori.

Burrow,hata hivyo, amezitaka jamii kulinda wanyama pori ili jimbo la Tana River liwe kivutio cha watalii na uwekezaji mbalimbali.

“Uwindaji haramu wa wanyama pori ni kizingiti hapa Tana River, sisi tunasema tuko na wanyama, lakini idadi ya wanyama wanao windwa ni kubwa kushinda sehemu nyingine ile nchini,’’ alisikitika Waziri.

Waziri wa Kaunti alisema hayo hapo jana, katika kikao cha kuhamasisha jamii kuhusu zoezi la kuhesabu kujao kwa wanyama pori kwenye Kounti.

Aliongezea kuwa katika kaunti jirani ya Garissa, mtu ataweza kuona wanyama pori kama pundamilia na wengine kwa sababu wana uhusiano mzuri na wanyama hao, akilalamika kuwa wakazi wa Tana River hawana uhisiano mwema na wanyama wa pori.

“Tumekuwa na mkutano na mkuu wa askari wa kaunti ili tuweze kuwapa mafunzo na askari wetu tukishirikiana na shirika la Shirika la Huduma kwa Wanyama Pori (KWS), ili kupiga doria katika sehemu zenye uwindaji haramu,’’ alisema Waziri Burrow.

Serikali ya kaunti ya Tana River imeanzisha zoezi la kutambua maeneo ya turathi za kitaifa ikishirikiana na hifadhi ya makavazi nchini (National Museum of Kenya), aidha zoezi la kutambua maeneo ya utalii ili kutathmini watawekeza wapi.

By Sadik Hassan

Leave a Reply