Friday, November 22, 2024
Home > Counties > Vijana Bungoma waungana  kutetea maslahi yao

Vijana Bungoma waungana  kutetea maslahi yao

Kundi linalojulikana kama Bungoma Youth Agenda (BUYA)  limewakashifu vikali wanasiasa waliowatumia vijana kusababisha machafuko katika uchaguzi mdogo uliokamilika hivi karibuni kule Kabuchai.

 

BUYA ni mrengo wa wanaharakati wa vijana na lengo kuu lake ni kutafuta malengo ya msingi na kuwaweka vijana kwenye nafasi za kisiasa, kiuchumi na katika jamii kwa ujumla.

 

Akizungumza na wanahabari mjini Bungoma,mwenyekiti wa wa mrengo huo Ignatius Nyukuri alisema kwamba kwa muda mrefu sasa vijana hawajatambuliwa na wamekosa umuhimu katika maswala ya kisiasa,kiuchumi na hata katika jamii kwa kukosa malengo na mwavuli mmoja wa kuwaleta vijana kwa pamoja kutimiza malengo yao.

 

Aidha aliongeza kwamba mrengo huo kwa sasa umefika katika kila wadi katika kaunti ya Bungoma ili kuwaleta vijana pamoja na sasa ina wenyekiti wanaosimamia kila wadi.

 

“Kila eneo bunge kwa sasa lina mwenyekiti anayetusaidia kukusanya na kuwaleta vijana katika mwavuli huu mmoja na chini ya wiki moja (BUYA) utakuwa mrengo unaokaririwa na kutajwa Bungoma nzima,” alisema Nyukuri.

 

Nyukuri aliongezea kwamba ajenda ya sasa ya mrengo huo ni kuhakikisha kwamba sodo zinawafikia wasichana, kushirikiana na kuwahimiza watahaniwa katika taasisi za elimu na kuandaa michezo ya kirafiki miongoni  mwa vijana hasaa wakati wa likizo refu inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

 

Ili kutimiza malengo haya Nyukuru amewaomba washikadau wanoshughulika na maswala ya vijana kushirikiana nao kwa pamoja ili kuweka msingi dhabiti kwa mpango huu.

 

Nyukuri alikashifu vikali madai kwamba kundi hilo la vijana linafadhiliwa na wanasiasa akisema kwamba hakuna mwanasiasa hata mmoja anayewawafadhili.

 

Alitaka idara ya jinsia,michezo na utamaduni katika kaunti ya Bungoma kuweka mpango wa kuwafaa vijana utakaowafanya wasikose lolote la kufanya hasaa kwa wale wasio na

na Khaemba Emmanuel/Lumwamu Roseland

Leave a Reply