Sunday, December 22, 2024
Home > Counties > Mwili wa mwanamke aliyepotea wapatikana

Mwili wa mwanamke aliyepotea wapatikana

Hali ya majonzi ilikumba wakazi wa eneo la Chandera katika gatuzi dogo la Molo leo wakati mwili wa mwanamke aliyetoweka ulipatikana kaitka shimo la maji taka.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 52 anayefahamika kama Martha Njeri alitoweka mnamo Oktoba 24 mwaka huu na shughuli za kumtafuta zimekuwa zikiendelea hadi jana asubuhi ambapo mwili wake ulipatikana ukiwa umefungiwa ndani ya gunia katika shimo la maji taka.
Kwa mujibu wa kakake marehemu Samwel Gitau, aliyezungumza na waandishi wa habari, ni afueni kuwa wmefanikiwa kupata mwili wa mpendwa wao ijapokuwa sehemu ya mwili wake kutoka kiunoni hadi miguuni haukuwepo.

Shughuli za kuopolewa kwa mwili wa Martha Njeri katika shimo la maji taka eneo la Chandera katika gatuzi dogo la Molo.

Isitoshe, Gitau alisema kuwa gunia lililokuwa na salio la mwili wa dadake lilikuwa limefungiwa kwa jiwe zito ili kuhakikisha kuwa mwili hautaelea lakini harufu ya uvundo uliotoka katika shimo lile ndio iliyowavutia wakazi kuangalia kilichokuwa ndani na kuupata mwili huo.
Hata hivyo, mkuu wa polisi wa eneo hili, Samuel Mukusi amethibitisha kisa hiki na kusema kuwa uchunguzi umeanzishwa na iwapo watakuwa na ushahidi utakaounganisha marehemu na mpenziwe basi hawatasita ila kumchukulia hatua ya kisheria.
Mukusi aliongezea kuwa wananchi walirudi mahala pa tukio na kutafuta sehemu ya mwili uliokosekana na kwa bahati nzuri ulipatikana baadaye.
Sehemu ya juu ya mwili wa Njeri pamoja na sehemu iliyopatikana baadaye zimepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya gatuzi dogo la Molo.

Na Emily Kadzo

 

Leave a Reply