Friday, November 22, 2024
Home > Counties > Makali ya bei ya bidhaa muhimu yaanza kushuka

Makali ya bei ya bidhaa muhimu yaanza kushuka

Watumiaji bidhaa muhimu waanza kupata nafuu kufuatia kuteremka kwa bei za bidhaa muhimu.

Uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la KNA mjini Kakamega umedhiirisha baadhi ya bidhaa kushuka bei zikiweko mafuta ya kupikia, mchele na sabuni ya kusafishia.

Akielezea hali hiyo, katika soko huru la Kakamega, mfanyibiashara Carolyne Were, alinadi kuwa bei ya mafuta ya kupikia lita kumi (10) imepungua hadi Sh 2000 ikilinganishwa na bei ya awali ya Sh 3200.

“Bei ya mafuta ya kupikia imepungua kutoka Sh 3200 hadi Sh 2000 kwa mtungi wa lita kumi, huku lita moja ya mafuta ikiuzwa rejareja kati ya Sh 230 na Sh 300,” alisema Bi.Were.

“Aidha bei ya mchele vilevile imeweza kupungua kutoka Sh 3000 kwa mfuko wa kilo 25, na kwa sasa hivi unauzwa kwa Sh 2500,” alisema huku aliongezea, “hali ambayo imedhiirisha kupungua kwa Sh 20 kwa kilo moja ya mchele kwa mnunuzi.”

Naye Mama Floridah Ambani, mmoja wa wauzaji sabuni alisema hivi: “Sabuni ya kusafisha ndio imeweza kushuka bei japo kwa kuzingatia aina ya sabuni, ambapo, baadhi ya sabuni zimeweza kushuka bei kwa kati ya Sh 50 na Sh 80.”

Hata hivyo, wafanyibiashara hao walilalama kuwa bei za bidhaa za kimsingi zingali ghali, hali ambayo inawapa wakati mgumu kuweza kumudu bidhaa hizo.

“Bei ya sabuni ya unga ingali bei ghali bila kusahau kwamba sabuni hiyo haina faida kubwa, hili linakuwa changamoto kwetu kama wafanyibiashara kwani inatupa wakati mgumu kuwashawishi kununua.bidhaa ya pamba chuma vilevile iko bei ghali  hali inayowalazimu wateja wetu kuinunua kwa bei inayopungua shilingi tano hivo kupata hasara sisi kama wafanyabiashara,” aliongeza  Floridah.

Kupungua huku kwa baadhi kunajitokeza baada ya tume ya kukusanya ushuru nchini KRA kurekebisha ushuru ili kufaa kiwango cha mfumuko wa bei za bidhaa nchini.

“Serikali yetu inapaswa kupunguza bei za bidhaa za kimsingi, kwa hiyo tunatarjia bei ya mafuta ya usafiri kupungua,” Floridah alisema.

Chama cha wazalishaji nchini almaarufu Kenya Association of Manufacturers (KAM) kwa baadhi ya hoja zilizotolewa mwezi mmoja uliotangulia,ilisema kuwa bei ya mafuta imeweza kuwa ikipungua kwa miezi michache iliyopita na mtindo huo unatarajiwa kutiliwa maanani  kwa kipindi cha miezi ijayo.

Ili kukidhi bei hii nafuu ya mafuta, serikali inaombwa na wanachama hawa kutupilia mbali ushuru uliowekwa na kupitia mimea [karanya na mazaaao ya mafuta] kwa kanuni za 2020.

Na Rose Adelaide

Leave a Reply