Tuesday, November 12, 2024
Home > Counties > Bungoma > Kilimo Kupigwa Jeki Bungoma

Kilimo Kupigwa Jeki Bungoma

Gavana wa Bungoma Kenneth Lusaka hii ametoa Hotuba yake ya kuhusu Hali ya Kaunti katika Bunge la Kaunti ya Bungoma.

Katika hotuba yake, Gavana Lusaka alimshukuru spika na waakilishi wa wadi kwa kumuunga mkono na idhini ya mawaziri wake katika kupitisha bajeti yake ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambayo kulingana naye iliwezesha utekelezwaji wa mipango ya maendeleo kuanza. .

Gavana Lusaka aliangazia ajenda yake ya kuleta mabadiliko katika idara ya Kilimo kwa kulenga kuongeza mchango ili kuathiri vyema pato linalopakana na uongezaji wa thamani, na kuimarisha ustahimilivu wa chakula katika Kaunti nzima.

Alitangaza uzinduzi na usambazaji wa ruzuku ya Mbegu na Mbolea kwa wakulima waliochaguliwa kuanzia Jumatatu, Februari 27 na kuongezea kwamba zoezi hilo litaanzia maeneo ya nyanda za chini ya Kaunti Ndogo ya Bumula na kuendelea hadi kaunti ndogo zote, zoezi litakalochukua wiki moja.

Lusaka amesema licha ya bajeti finyu msaada wa waakilishi hao wa wadi kupitisha bajeti ya ziada ulimuezesha kuongeza idadi ya watakaonufaika na ruzuku kutoka familia 200 kwa Kila wadi hadi familia 500 katika mwaka huu wa mwisho wa fedha.

Kulingana na Lusaka, kaunti hiyo sasa itakuwa na jumla ya familia 21,900 zitazonufaika na mpango huo ambao ni ongezeko kubwa sana kutoka kwa familia alfu tisa (9000) zilizonufaika hapo awali.

Aliongezea kuwa Kila familia inayonufaika inastahili kupata ekari Moja pekee ambayo itajumuisha mfuko mmoja wa kilo 50 wa mbolea ya kupandia, mfuko mmoja wa kilo 50 wa mbolea ya kukuzia, na mfuko wa kilo 10 wa Mbegu zilizoidhinishwa.

Ili kuongeza na kukidhi mahitaji ya uzalishaji wa kichinjio cha Chwele, Lusaka alisema utawala wake unanuia kuzindua kampeni ya ‘fuga kuku’ Ili kuhamasisha wakaazi wa mashambani katika Kaunti nzima katika kukuza kuku kwa madhumuni ya kibiashara.

Katika Elimu, Lusaka ilisema kuwa mchakato wa kurahisisha mchakato wa Scholarship unakaribia kukamilika.

Hata hivyo alikiri kupokea kesi kadhaa za rufaa ambazo timu ya wafadhili bado inafanya ucjinguzi.

Kwa mujibu wa mwongozo uliowekwa katika Mpango wa Usaidizi wa Elimu wa Kaunti ya Bungoma, Serikali ya kaunti imeanza kuoanisha mgao huo na mpango wa Bursary pamoja na mpango wa ufadhili wa masomo kwa madhumuni ya kufuata.

Shillingi millioni 4 zilitengwa kwa kila Kata kwa ajili ya kusimamia mpango wa basari huku asilimia moja ikiendea shule za sekondari VTCs.

“Mgao huu ukigawanywa kwa kiasi cha kshs 5000 kwa kila mwanafunzi unashughulikia wanafunzi 36000 katika Kaunti nzima. Ninazihimiza kamati za wafadhili za kata kupendelea familia zote za watoto yatima na zinazoongozwa na watoto kwa mgao mkubwa inapowezekana,” alisema Lusaka.

Katika idara Barabara na miundombinu, Lusaka alibainisha hatua kubwa zilizopigwa kwa kipindi ambacho amekuwa afisini, na kueleza kuwa Uongozi wake umetoa zabuni ya miradi mipya 94 ambayo ina barabara 89 na kalvati 5 zilizosambaa katika wadi zote, huku kila wadi ikiwa na angalau miradi miwili.

Alitoa mfano barabara ya Lusaka na barabara ya Kaberwa-Chebkitale kuwa wakandarasi wanafanya kazi.

Gavana Lusaka amesema serikali ya kaunti itashirikiana na Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu ya Kenya KENHA katika ujenzi wa barabara ya makutano katika eneo la kanduyi.

Lusaka amesema mafanikio makubwa yamepatikan katika sekta ya afya kwa kuthibitishwa kwa wahudumu 179 wa afya kutoka kandarasi. Vile vile alikiri kuboresha sekta ya utali na Biashara, miongoni mwa miradi nyingine

Na Douglas Mudambo

 

Leave a Reply