Sunday, December 22, 2024
Home > Counties > Kijana ajitia kitanzi

Kijana ajitia kitanzi

Mvulana mmoja wa umri wa miaka 12 amejitia kitanzi katika mtaa wa Kasarani eneo la Elburgon.
Tukio hilo lilimewaacha wengi vinywa wazi kwani mwendazake anayefahamika kama Laban Kimungu hakuonyesha dalili zozote za kutaka kujitoa uhai.
Kamanda wa polisi wa gatuzi hilo dogo, Samuel Mukusi alithibitisha kisa hicho akisema kuwa polisi wameanzisha uchunguzi kutathmini kiini cha tukio hilo.
Inasemekana kuwa, Kimungu katika usiku wa kuamkia leo aliwaacha wazazi wake pamoja na nduguze sebuleni kabla ya kujiua.
Wazazi wake, Paul Muiruri na Hellen Wanjiku waligubikwa na simanzi wasijue lililomtatiza mwanao wa darasa la tano kwani hakuacha kijibarua chochote kusema yaliyomsukuma kujitoa uhai.
Mwili wa Kimungu ulipatikana ukining’inia katika paa la chumbani mwake lakini mpango ulifanywa kuupeleka mwili wake katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Nyayo mjini Elburgon.

Na Emily Kadzo

Leave a Reply