Monday, December 23, 2024
Home > Counties > Nakuru > Wanaohatarisha maisha ya watoto waonywa

Wanaohatarisha maisha ya watoto waonywa

Mbunge wa Molo, Kuria Kimani ameitaka idara inayoshughulikia maswala ya watoto katika maeneo ya Molo na Rongai kuwachukulia hatua kali wale wanaonyanyasa watoto wa shule kimapenzi.

Bwana Kimani alitoa wito huo kufuatia kuongezeka kwa malalamishi kuwa watoto wa umri wa chini ya miaka 18 wanajihusisha na ngono za mapema na kisha kuambukizwa virusi vya Ukimwi hasa maeneo ya Salgaa na Sachangwan.

Aidha, Mbunge huyo alidokeza kuwa swala hilo limechangiwa mno na madereva wa masafa marefu wanaowashawishi hao watotot kwa kuwapa pesa ili kuburudika nao wakati wa mapumuziko.

Kimani alitaka serikali kushugulikia swala hilo kwa kikamilifu ili watoto wawezo kuzingatia masomo yao.

Hata hivyo, Kimani amependekeza msako kufanywa na Idara hiyo wakishirikiana na maafisa wa polisi ili kuwachukulia hatua kali wanaowaharibia watoto hao Maisha ili iwe funzo kwa wengine walio na tabia kama hiyo.

Aliwaonya wazazi dhidi ya kutumia watoto wa kutafuta pesa kutoka kwa madereva hao huko akiwataka madereva hao kuacha tabia ya kutumia peza zao kuwalaghai watoto wa shule.

Aliwaomba wazazi kujizatiti na kutafuta mbinu badala za kujikimu kimaisha ili watoto wapate fursa ya kwenda shule kwa ajili ya Maisha yao ya siku za usoni.

Aliwataka wazazi kukuza maadili mema kwa watoto wao huko akiwashauri kuonyesha mifano miema kwao ili waeze kuwaiga popote wakapokuwa.
Na Emily Kadzo

Leave a Reply