Friday, November 22, 2024
Home > Counties > Maji taka yaathiri wakaazi wa Zimmerman

Maji taka yaathiri wakaazi wa Zimmerman

Wakaazi wa Zimmerman wamelalamikia mfumo duni wa mifereji na majitaka yanayoathiri biashara yao, afya na usafiri haswa wakati wa mvua.

 

            Kulingana na Veronicah Wanjiru, mkaazi na mfanya biashara wa eneo la Zimmerman katika mahojiano na shirila la habari la KNA alisema, “Majitaka huenea hadi kwenye barabara na hata kwenye maduka ya kuuzia bidhaa wakati ambapo mvua imenyesha. Anahofia kuwa hali ya anga inapozidi kubadilika na mvua ipate kuendelea kunyesha, mazingira yataathiri biashara yao ambayo ni tegemeo lao.

 

“Wiki iliopita, mvua iliponyesha, maji taka yaliingia dukani mwangu na kuathiri takribani asilimia arubaini ya bidhaa ambazo nilitumai kuuza ili niweze kujikimu kimaisha. Kuta ziliathirika pakubwa kwani maji yale yaliacha alama ya uchafu na inabidi nipake rangi katika duka langu.  “Alisema hivi akiashiria kwa kidole alama ambayo maji yale yaliwacha.

 

“Isitoshe wakati wa masika, ni nadra kupata wateja kwani ni vigumu sana kutembea katika eneo hili baada ya mvua kunyesha. Hii ni kwa sababu baada ya mvua, maji husambaa hadi kwenye barabara na kutiririka kwa mwendo kasi isiyo ya kifani.

 

            Niliwasilisha malalamishi ya hali duni yaliyosababishwa na maji taka yaliyokuwa futi tano nje ya biashara yangu kwa mwenye nyumba bwana Johnstone Muchina ila tu jibu nililopata ilikuwa,“Hili ni jukumu la wakaguzi wa baraza la Kaunti ya Kiambu.”

 

            Mita chache kando ya biashara ya Bi. Wanjiku kulikuwa na banda la mboga la Bwana Paul Kinyanjui. Katika mahojiano na KNA, Bwana Kinyanjui alisema, “Kutokana na majitaka haya, kumekuwa na ongezeko la suala la afya. Hii ni kwa sababu ndani ya majitaka yapo mabomba ya maji yanayosafirisha maji safi ya matumizi nyumbani. Wakati mwingine, mabomba haya ya maji safi hupasuka na maji machafu ya maji taka huchanganyika na maji masafi. Watu huishia kunywa maji yaliyochafuka na kuadhirika kiafya bila mtetezi”alisema huku akimwonyesha mwandishi huyu hasara aliyokadiria.

 

            Nimefanya uchunguzi kimakinifu na kuona watu wa kazi mtaani wanaokuja kufanya usafi katika eneo hili. Ila ni kwa masikitiko kuona hakuna jambo lililofanywa kuzuia maji yale ya taka kwa kufurika baada ya mvua kunyesha.

 

Alihoji kuwa Kinachofanyika ni kwamba hao Vijana walioanza kufanya kazi katika mitaa ya mabanda mwezi wa sita mwaka jana, wao huondoa plastiki na vifaa vya taka vilivyotupwa na wapita njia kwenye maji ili kuyapatia nafasi yasifurike. Ukiangalia mazingira yenyewe, taka inazidi kuongezeka na kuidhoofisha mazingira.

 

            Zaidi ya hayo, kando ya majitaka yale vimo vifaa vya taka vinavyosababisha harufu mbaya. Miongoni mwa vifaa hivi ni vijikaratasi vya plastiki, mboga zilizooza, nepi zilizotumika na hata vyakula vilivyoharibika. Bwana Kinyanjui akitamatisha kauli yake alisema, “Ni jukumu la kila mkaazi kuhakikisha kwamba amehifadhi mazingira kuzuia kuenea kwa magonjwa kama kipindupindu.

 

            Juhudi za mwanahabari huyu kupata suluhu ya wakaazi wa Zimmerman kutoka katika ofisi ya Afya ya Kitengo cha Kaunti ya Kiambu hazikufanikiwa kwa vile hakukuwa ofisini.Nambari yake ya simu pia haikujibiwa hata  baada ya kujaribu kumfikia kwa muda wa masaa mawili.

 

Na Lydia Shiloya na Miriam Muli

           

Leave a Reply