Janga la ugonjwa wa corona limeleta mabadiliko makuu katika Kaunti ya Kiambu na baadhi ya wakaazi wa eneo la Ruiru wameweza kufuatilia amri za kujikinga kutokana na ugonjwa huu ijapokuwa kuna changamoto tele.
Wakaazi wa Ruiru wanafuata amri ya serikali ya kutotoka nje ifikapo saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi ili kuepuka maambukizi ya ugonjwa wa korona.
Amri hii ya kutotoka nje kuanzia saa moja usiku imeweza kuwaadhiri pakubwa wafanyi biashara wadogo wadogo. Hii ni kwa sababu wanafaa kufunga maduka na sehemu zao za biashara kabla ya saa kumi na mbili ili waweze kufika makwao ifikapo saa moja usiku.
Mary Wambui mfanyi biashara wa duka la dawa alikuwa na machache ya kusema; “Kuna changamoto kwetu wafanyi biashara. Hii ni kwa sababu biashara kama hii yetu ya madawa inategemewa sana na wakaazi wa eneo hili. Kumbuka kuwa ugonjwa au maumivu haina wakati.” Wambui alisema.
Aliongezea kwa kusema kwamba ikifika masaa ya jioni wanunuzi wake wanapungua ili waweze kuwa nyumbani kabla ya saa moja. Wambui aliongeza kusema kuwa kuwa hapati mapato ya kutosha na faida yake inakuwa chini sana jambo ambalo si nzuri katika sekta ya biashara.
Amri hii ya wananchi kuwa nyumbani saa moja jioni hadi saa kumi na moja asubuhi ilitokana na tangazo la Rais Uhuru Kenyatta ili kwamba wakenya waweze kuzuia maambukizi.
Na Juliet Mung’ara and Lydia Shiloya