Friday, November 22, 2024
Home > News > Wanaokagua ubora wa mijengo watakiwa kuboresha kazi yao

Wanaokagua ubora wa mijengo watakiwa kuboresha kazi yao

Chama cha walimu KNUT, kimeomba idara ya kukagua ubora wa mijengo katika shule kuongeza juhudi zao ili kuepusha majanga ambayo yameshuhudiwa hivi karibuni katika shule kadhaa nchini.

Katibu wa chama hicho katika Kaunti ya Vihiga, Maurice Chalenga amesema kwamba hatua hiyo itachangia kuimarisha usalama wa walimu pamoja na wanafunzi wakiwa shuleni.

Huku akitaja kisa cha wiki jana kilichotokea katika shule ya Msingi ya Kakamega kilichochangia wanafunzi kumi na wanne kupoteza maisha yao huku wengine wakiwachwa na majeraha, Chalenga amesema kwamba majumba mengi katika shule nyingi humu nchini hayana ubora unaostahili.

Alinena kwamba masomo ya bure nchini na juhudi za serekali za kuhakikisha kwamba wale watahiniwa waliokalia mtihani wa darasa la nane mwaka jana wamejiunga na shule za upili kwa asilimia mia moja imeleta shinikizo kwa miundo msingi katika shule nyingi.

Kutokana na hayo, Katibu huyo ameitaka serikali kuu kutoa fedha za kutosha kwa shule za umma zitakozotumika kwa ujenzi wa madarasa na mijengo ifaayo.

Na  Isaiah  Nayika

Leave a Reply