Monday, December 23, 2024
Home > Education > Matayarisho ya mitihani ya kitaifa yakamilika

Matayarisho ya mitihani ya kitaifa yakamilika

Matayarisho kwa mitihani ya kitaifa katika Kaunti ya Vihiga yamekamilika.

Haya ni kulingana na afisa anayesimamia masomo katika Kaunti hiyo, Bi Hellen Nyang’au.

Akiongea na Shirika la KNA, Nyang’au alidokeza kwamba zaidi ya watahiniwa elfu 15 wa shule za upili na elfu 17 wa shule za msingi wanatarajiwa kukalia mitihani hiyo.

Nyang’au alieleza kuwa mipangilio yote ikiwemo usalama na hata maswala ya usafirishaji wa vifaa vitakavyotumika wakati wa mitihani hiyo, imekamilika.

Kwa upande mwingine, Bi Nyang’au ameonya kwamba serikali imejiandaa vilivyo kukabiliana na yeyote yule ambaye ako na mipango ya kuleta vurugu popote pale na hata kuiba mitihani hiyo.

Aliongeza kwamba hakuna mwalimu mkuu yeyote ataruhusiwa kusafirisha mitihani hiyo kibinafsi pasipo kutumia magari ambayo imeidhinishwa na ofisi yake.

Mitihani ya darasa la nane imepangiwa kung’oa nanga siku ya kesho kote nchni, huku ya kidato cha nne ikifuata baadaye.

Na  Isaiah Nayika

Leave a Reply