Monday, December 23, 2024
Home > Education > Ajitia kitanzi kwa hamaki ya kutotaka kufuata maagizo

Ajitia kitanzi kwa hamaki ya kutotaka kufuata maagizo

Mvulana mmoja wa kidato cha kwanza eneo la Mau Summit, katika gatuzi ndogo la Molo amejitia kitanzi kwenye mti.

Inakisiwa kuwa mwendazake ambaye ni mwanafunzi katika shule ya upili ya Mau Summit aliwakwepa waliojaribu kuyaokoa maisha yake.

Kwa  mujibu wa kakake marehemu, Salim Lang’at, nduguye alikanywa dhidi ya kuachilia ng’ombe wao kula mimea ya mahindi na ni hapa alipandwa na mori na kutaka kumkatakata Langat.

Vurugu lilizuka akikanywa zaidi kutomuangamiza Langat kwa kutumia panga alilokuwa nalo lakini aliposhindwa nguvu, alimfungua ng’ombe na kutorokea shambani akiwa ameibeba kamba ile.

Wakati huu, walijawa na wasiwasi na kuamua kumkimbiza alikokimbilia lakini kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha, walimpoteza na kisha baadaye kupata taarifa kuwa mwili wa mwendazake ulipatikana ukining’inia mtini.

Ama kweli, wakaazi wamepigwa na butwaa kutokana na hatua aliyoichukuwa kijana huyu wanayemfahamu vyema kama mnyamavu na asiye na kinyongo na yeyote yule.

Hata  hivyo, Chifu msaidizi wa eneo la Sarambei, Joseph Ng,eno alithibitisha kisa hiki akiwasihi wazazi walio na watoto wa umri huu kuwa na mazungumzo mara kwa mara ili kuimarisha uhusiano mwema hata wakati ugomvi unapozuka, inarahisisha njia mbadala za kupata suluhu.

Mwili wa kijana huyu wa umri wa miaka 14 ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya gatuzi ndogo la Molo.

Na  Emily  Kadzo

Leave a Reply