Monday, November 25, 2024
Home > Counties > Uzinduzi wa miradi katika sekta ya afya Pokot Magharibi

Uzinduzi wa miradi katika sekta ya afya Pokot Magharibi

Serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi imechukua hatua katika kuzindua miradi iliyokamilika kwa lengo la kusaidia wananchi mashinani

Gavana Simon Kachapin alisema katika maono yake ya kuhudimia wananchi miaka mitano ijayo ni kuhakikisha kwamba wananchi katika kaunti yake wanapokoea huduma kwa ukaribu.

“Siku ya leo nimeweza kuzindua miradi minne katika wadi ya Chepareria ikiwamo zahanati ya Senetwo, Propoi na chumba kuu cha uzazi katika maeneo ya Ywalateke,” kasema Kachapin.

 “Ninashukuru kwa sababu hii ni baadhi ya maono yangu katika kutumikia wananchi wa Westp Pokot miaka tano ijayo,” kaongeza gavana.

Alisisitiza kuwa lengo kuu la shirika la Afya Ulimwenguni linaeleza kuwa ni lazima wananchi wapate huduma kwa ubali usiopita zaidi ya kilomita 5 huku lengo lake likiwa kuafikia ipasavyo.

“Tuko na jukumu kama magavana kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma kwa ukaribu kwa sababu ni jambo ambalo limefanyiwa ugatuzi,” alisema Gavana.

Kachapin alitaja kuwa kuna miradi zaidi ya 42 ambayo anapanga kuzindua hivi karibuni ili kuhakikisha kwamba maeneo yote ya mashinani wanapokea huduma kwa ukaribu.

Gavana aliahidi kuwa watashirikiana na serikali kuu kuhakikisha sera wanayopeana wanaitekeleza kwa kikamilifu.

Amerai wenyeji kutumia nafasi hii katika kuhakikisha kwamba miradi hii inatumika kwa njia inayohitajika akitaja kuwa kujifungua nyumbani ni jambo ambalo halikubaliwi na ni hatari mno.

“Ningependa kina mama wetu watumie nafasi hii haswa katika kupokea mafunzo kuhusu lishe bora na hata mbinu mwafaka ya kulea watoto wadogo,” Gavana aliongeza.

Naibu wake Chifu Japheth Rutto alitoa shukrani zake kwa Gavana katika kuwaletea chumba kuu cha uzazi akisema kuwa awali ilikuwa tu zahanati huku kina mama wakilazimika kutembea mwendo mrefu kutafuta huduma.

“Wazo la Gavana la kuleta chumba cha uzazi sehemu hii limekuwa la manufaa mno,” Chifu alisema.

Alisifu utendakazi wa Gavana akieleza kuwa tangu ugatuzi uanze, serikali ya kaunti imerahisisha mambo mengi haswa katika sekta ya afya.

Alisihi wananchi wote kutangamana na Gavana na pamoja na serikali ya kaunti katika kushirikiana kwa pamoja ili wapate kusonga mbele kimaendeleo.

Aidha wakazi walieleza kuwa idadi kubwa ya watu katika maeneo ya Ywalateke ndio iliyochochea kujengwa kwa hospitali sehemu hio

Alitoa shukrani zake kwa serikali ya kaunti kwa kuitikia wito wa wananchi katika kuwajengea zahanati ambayo itasaidia watu wengi sehemu hio.

Aliomba serikali kuendeleza juhudi za kuongeza madaktari ambao watasaidia katika kutoa huduma kwa haraka na kwa njia inayofaa.

Hata hivyo kina mama walitoa shukrani zao wakieleza kuwa kina mama wengi walikuwa wakijifungua mitaani ambayo ni hatari, wakihimiza kila mmoja atembee kule zahanatini kwa minajili ya kupata huduma.

Aidha wameomba madaktari kuajiriwa ikiwamo wale wa Lishe Bora ili kuwapa mafunzo kina mama kuhusu ulezi bora na pia mbinu bora ya kunyonyesha watoto. Zaidi, kina mama wanataka kujengewa maabara ambayo itatumika katika kupima damu

Na Anthony Melly na Agneta Chebet

Leave a Reply